Murang'a: Polisi Wamkamata Baba wa Mtoto Aliyenaswa Kwenye Video Akiendesha Prado
- Ayub Kinyanjui Muigai alikamatwa katika eneo la Gatanga na maafisa wa trafiki kutoka Kikwara
- Kinyanjui atakabiliwa na mashtaka ya kumruhusu mtu asiyekuwa na leseni kuendesha gari
- Baba huyo anatazamiwa kufikishwa kortini hii leo Jumanne, Juni 15
Habari Nyingine: Siwezi! na Siwezi! Rais Uhuru Akataa Katakata Kuidhinisha Majaji Sita Waliosalia
Maafisa wa polisi wamemkamata baba wa mtoto ambaye alinaswa kwenye video akiendesha gari aina ya Toyota Prado TX katika eneo la Delview Park mjini Thika.
Katika video ambayo ilisambaa mtandaoni Jumapili, Juni 13, mvulana huyo anaonyeshwa akiendesha gari lao bila wazazi kuingiwa na wasiwasi wowote.
Kulingana na ripoti ya polisi, Ayub Kinyanjui Muigai alikamatwa katika eneo la Gatanga na maafisa wa trafiki kutoka Kikwara wakishirikiana na makachero wa DCI.
Habari Nyingine: Ayub Muigai: Video ya Mtoto wa Miaka 8 Akiendesha Prado Yawasha Moto Mtandaoni
Kinyanjui atakabiliwa na mashtaka ya kumruhusu mtu asiyekuwa na leseni kuendesha gari.
Baba huyo anatazamiwa kufikishwa kortini hii leo Jumanne, Juni 15.
Kinyume na mataifa mengine kama vile Marekani ambapo watoto wanaruhusiwa kuendesha gari wakiwa na umri wa miaka 14, nchini Kenya ni lazima mtoto atimie umri wa miaka 18 kabla ya kupewa leseni ya kuendesha gari.
Habari Nyingine: Maajabu ya Dunia: Mvuvi Asimulia Alivyonusurika Kifo Baada ya Nyangumi Kummeza Kisha Kumtapika
Sheria zingine za trafiki
Endapo umefuzu kwa mara ya kwanza kutoka shule ya kuendesha gari na kukosa kuonyesha kwa kuweka ishara ya "L" mbele na nyuma ya gari lako, basi utalipa faini ya Ksh. 1,000.
Unatakiwa kuwa na vyeti vyako vya bima kila wakati unaposafiri endapo utapatikana bila vyeti hivyo waweza kufungwa jela miaka kadhaa ama kulipa faini ya Ksh.100,000.
Ukikosa kubadilisha leseni yako ya kuendesha gari baada ya siku inayohitajika utalipa faini ya Ksh.1,000.
Endapo utapatikana ukiendesha Nissan, matatu ama basi ambalo halijachapishwa vyema barabara ya shughuli zake utalipa faini ya Ksh. 5,000.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZoJ2fpZmp6ikmai2bsPApqKapZGprm6uwJuYZq%2BRYrq1u9OoZJqkma6ytK3Mm5iaZZ2pu6WtzqJkmqOZo7K0tMBmp6uZlKR7qcDMpQ%3D%3D