Mwimbaji Kambua Manundu aomboleza kifo cha mtoto wake
- Kambua amefiwa na mtoto wake wa pili siku chache baada ya kuzaliwa
- Kulingana na ujumbe wake kwenye mtandao wa Instagram, Kambua alisema atamkosa sana mtoto huyo lakini yote ilikuwa ni mpango wa Mungu
- Kambua alikaa katika ndoa kwa miaka saba kabla ya kujaliwa mtoto wake wa kwanza ambaye kwa sasa anaelekea umri wa miaka mitatu
Mwanamuziki na mtangazaji maarufu Kambua Manundu anaomboleza kufuatia kifo cha mtoto wake mchanga, Malachi Manundu Muthiga.
Habari Nyingine: Atwoli atamani kuikamata shingo ya ERC kwa kuongeza bei za mafuta: "Wakenya wamechoka"
Habari Nyingine: Seneta Mohammed Yusuf kuzikwa alasiri katika makaburi ya waislamu ya Lang'ata
Kupitia mtandao wa Instagram, Kambua alisema yeye pamoja na familia yake walimpenda Muthiga lakini Mungu alimpenda zaidi na ndio sababu alimchukua na kwa hivyo hangekosoa uamuzi wa Mungu.
Aidha, Kambua aliwaomba mashakiki wake wampe muda wa kuomboleza kifo cha mtoto wake ambacho kilitokea ghafla baada kuzaliwa siku chache zilizopita.
" Ulikuwa unapendwa sana na tutazidi kukumbuka, mama yako, kakako pamoja na babako yako walikuwa wanakupenda na watakukosa sana," Kambua alisema.
TUKO.co.ke inafahamu kuwa Kambua alikuwa anatarajia mtoto wake wa pili na alikuwa amempatia majina Malachi Manundu Muthiga.
" Malachi sasa hana maumivu tena na hatapata matibabu yoyote hapa duniani, hatuwezi yazuia machozi yetu kwa sababu tulimpenda sana na hatungeweza kuelezea upendo wetu kwake. Lakini kwa imani hatutatikisika kwa vile tunamwamini Mungu wetu," Aliongezea Kambua.
Kambua aliishi katika ndoa kwa zaidi ya miaka saba kabla ya kubarikiwa mtoto, hata hivyo hakuwahi kataa tamaa lakini alizidi kumuomba Mola abariki tumbo lake la uzazi.
Mwaka mmoja baada ya kujaliwa kifungua mimba, Kambua alipata mimba ya pili lakini mipango ya Mungu huwa ni ya ajabu, alimchukua mtoto huyo siku kadhaa baada ya kuzaliwa.
Kwenye ujumbe wake, Kambua anaonekana kumshukuru Mungu kwa hatua hiyo na amesema mipango yake sio ya kukosolewa.
Mashabiki wake mitandaoni wamemtumia rambi rambi zao na kumtaka azidi kuwa mwenye nguvu na matumaini kwamba Mungu atambariki na mtoto mwingine.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZYBxfJZmpLChnZeuq7WMpJimmqWWeq6tza6lna1dlryurs6lnLOZXaC2p7uMnJ%2BaZZ2pvLW7jLCYpJ1encGuuA%3D%3D