Raila Odinga afanya kikao cha dharura na maafisa wakuu wa ODM
- Waandishi wa habari walifungiwa nje ya mkutano huo uliofanyika Convent International Hotel
- Agenda ya mkutano huo haijabainika ila inadaiwa mengi yalizungumzwa ikiwemo siasa za ugavana wa Nairobi
- Chama hicho cha upinzani kilikishutumu chama tawala cha Jubilee kwa kukosa kukosa kutimiza maafikiano ya handisheki
Kinara wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga ameandaa mkutano wa dharura na maafisa wakuu wa chama hicho kutoka kaunti zote 47.
Waandishi wa habari walifungiwa nje ya kikao hicho kilichofanyika Jumanne, Januari 19, ambacho kiliandaliwa katika hoteli ya Convent International.
Habari Nyingine: Sababu iliyofanya nimpe Diamond jina la baba feki, Mama Dangote
Haijabainika agenda kuu ya mkutano huo ilikuwa ni nini ingawaje fununu zinasema kulikuwepo na mazungumzo ya madai ya usaliti wa Jubilee na vile vile siasa za atakayerithi kiti cha Ugavana Nairobi.
Inasemekana ODM inataka mmoja wa wanachama wake ateuliwe ili awe naibu gavana wa Anna Kananu Mwenda.
Chama hicho cha Upinzani kimesuta vikali kile tawala kwa kukosa kuwajibikia makubaliano yao wakati wa handisheki.
Habari Nyingine: Mzee afariki dunia baada ya kurambishwa asali na kipusa usiku kutwa
Kumekuwepo na uvumi kwamba handisheki inaporomoka kutokana na vita ambavyo baadhi ya wanasiasa wa ODM wamekuwa wakiipiga serikali.
Hivi majuzi, Seneta wa Siaya James Orengo alimsuta vikali Rais Uhuru Kenyatta kwa namna aliyoendesha serikali huku akimtaka kuilainisha serikali yake.
Naibu Rais William Ruto naye alifai kwamba aliyekuwa Waziri Mkuu anapanga kuitoroka handisheki na kisha kukiwacha chama cha Jubilee kikiwa kimegawanyika.
“Ruto alimshutumu vikali Raila ambaye aawali alikuwa akiikosoa mara kwa mara serikali kwa kutotimiza ahadi zake wakati wa kampeni akisema kuwa tangu kinara huyo wa ODM alipoingia serikalini miradi mingi imekwama,” Rauto alisema.
Read: ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZX1zgpFmqZqhnJZ6sLDIp56aZZGbrq%2FFwGaioqORpHqktMBmm6GZoqq%2FonnNmmSmmZGbtrStjLCYpK2lYsSiec6dpGegpKK5