Mwimbaji Ruth Matete aomba msaada zaidi baada ya kumzika mumewe
-Apewajoye aliaga dunia Aprili 11 akipokea matibabu KNH baada ya ajali iliyomwacha na majeraha mabaya
-Marehemu alizikwa katika makaburi ya Lang'ata siku ya Alhamisi
-Awali, Matete alikuwa amewaomba wahisani kumsaidia kulipa gharama ya matibabu na mazishi
-Ruth pia aliwashukuru wahisani kwa maombi na mchango wao kifedha na jumbe za kumtia moyo
Mwimbaji wa nyimbo za injili Ruth Matete, amewaomba Wakenya kuendelea kumsaidia pamoja na mwanawe kufuatia kifo cha ghafla cha mume wake.
Ruth, alimpoteza mume wake John Olakami Apewajoye, katika ajali mbaya ya mlipuko wa gesi nyumbani kwao jijini Nairobi mnamo Aprili.
Habari Nyingine: Mbunge Babu Owino atangaza sasa ametengana na pombe na kuokoka
Habari Nyingine: Betty Bayo atangaza kuhusu mchumba wake mpya
Marehemu Blessed John Olakami Apewajoye alizikwa katika makaburi ya Lang'ata siku ya Alhamisi, Julai 23.
Awali, Matete alikuwa amewaomba wahisani kumsaidia kulipa gharama ya matibabu na mazishi iliyorundikana kutokana na mwili wa mumewe kuhifadhiwa kwa miezi minne katika makafani ya Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.
Habari Nyingine: Ruth Matete amzika mumewe
Ruth pia aliwashukuru wahisani kwa maombi na mchango wao kifedha, kumpigia simu na kumtumia jumbe za kumtia moyo.
“Asanteni sana kwa mchango wenyu kifedha, kwa maombi, simu na jumbe na njia zote ile mlisimama nasi.Hamtawahi kukosa. Na Mungu awazidishie,”
"Bado nambari ya mchango haijafungwa, lakini endapo ungependa kutuma msaada kwa mtoto Toluwa na mimi, waeza kunitumia kwa nambari yangu ya M-Pesa, 0706206840.Tafadhali tuendelee kusimama na Toluwa na mimi katika maombi kwa safari iliyoko mbele yetu.Najua Mungu atatuwezesha," alisema Ruth.
Apewajoye aliaga dunia Aprili 11 akipokea matibabu KNH baada ya ajali iliyomwacha na majeraha mabaya ya kuchomeka kutokea nyumbani mwao.
Wawili hao ambao walifunga ndoa Novemba 2019 walikuwa wanamtarajia kifungua mimba wao wakati mkasa huo ulitokea.
Ubalozi wa Nigeria nchini Kenya uliagiza mwili wake Apewajoye uzuiliwe kwa muda hadi pale ambapo serikali ya taifa hilo itatoa taarifa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbH11hJRmpLChnZeuq7WMq6ytoF2irrWx055kmqedl65uudKamJ2ZXa%2BuqrDIZpmamZSWerqtjKSsprKZoK5uudSmnLCdXp3Brrg%3D