Wanasiasa wanafanya mikutano usiku kupanga mikakati, Kabogo asema
- Kabogo ameonya wanasiasa kuwa 2022 mambo yatakuwa tofauti kwenye debe
- Alisema Wakenya wamekerwa na hulka za wanasiasa ambao wanarindima siasa wakati ambapo kuna majanga ya mafuriko na covid-19
- Alikemea kelele zinazoskika ndani ya Jubilee na kusema Rais apewe nafasi kuendesha ajenda yake
Aliyekuwa gavana wa Kiambu William Kabogo amewataka wanasiasa wakome kurindima siasa wakati huu Wakenya wanapitia majanga.
Kabogo alisema licha ya kuwa Wakenya wanaandamwa na matatizo chungu nzima, viongozi wamewaacha kuhangaika peke yao.
Habari Nyingine: DP Ruto aomboleza kifo cha nduguye Wetangula
Alisema anakerwa sana kuwa kuna kundi la wanasiasa ambao wanashiriki mikutano ya usiku kupanga njama za kisiasa.
"Watu wanakufa njaa na wengine kwa sababu ya mafuriko na wanasiasa wajinga ni kuzungumza tu siasa.
Tunazunguka usiku wakati huu wa kafyu tukiulizana sijui tufanya nini, sijui ni wapi tutafanya nini. Ushenzi mtupu," alisema Kabogo
Habari Nyingine: Meru: Afisa wa polisi apatikana ameaga dunia baada ya kukorofishana na mkewe
Aliwataka Wakenya waambie viongozi kuwa wamechoka na siasa na kile wanataka kwa sasa ni huduma ili waweze kujikimu.
"Wakenya tuambieni viongozi wawache kufikiria mambo ya uchaguzi. Uchaguzi utakuja na kuisha," alisema Kabogo.
Kabogo alisema Rais Uhuru Kenyatta anafaa kupewa nafasi ya kutekeleza ajenda zake ndani ya miaka miwili iliyosalia.
Habari Nyingine: Tuju sasa amtambua DP Ruto, asema Jubilee haitavunjika
Kabogo aliyasema hayo kupitia video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook Jumamosi, Mei 16.
"Nataka pia niambie viongozi kuwa wakati huu wa kupiga kura mtashangaa. Hawa Wakenya wamejipanga chini ya maji kwa sababu sisi viongozi tumewaangusha," aliongeza Kabogo.
Kumekuwa na joto la kisiasa ndani ya serikali ya Jubilee haswa baina ya wandani wa Rais na wale wa naibu wake William Ruto.
Habari Nyingine: Athi River: Kijogoo atimuliwa na shuga mami usiku
Kumeibuka mirengo ya Tangatanga na Kieleweke kati ya wale wanaounga mkono Uhuru na wale wa Ruto.
Makundi hayo yamekuwa yakiongeza joto la kisiasa humu nchini kila upande ukivuta ngoma upande wao.
Kutimuliwa kwa aliyekuwa kiongozi wa wengi seneti Kipchumba Murkomen na kiranja Susan Kihika kumeongeza kasi kwenye moto unaochoma Jubilee.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaoR1fZhmrpqmkai2or%2FAZq6appGbrq%2FFwGakoqOlqa6vu4yuqqKjpWK4trzAp56aZZ2euKK3wK2gZqORl7you4yaqp6lkWO1tbnL