Moi alipenda kuangalia mieleka na alikuwa shabiki mkubwa wa Big Daddy
Wakati wa uhai wake marehemu rais mstaafu hayati Mzee Daniel arap Moi licha ya kuipenda kazi yake sana akiwa Kiongozi wa Taifa, aliipenda familia yake sana na kila mara alitenga muda kuwa na watoto wake.
Habari Nyingine: Fahamu jinsi mazishi ya Mzee Moi yatakuwa tofauti na ya makabila mengine ya Kalenjin
Haya yalifichuliwa Jumanne, Februari 11 na Seneta wa Baringo Bw. Gideon Moi, wakati wa ibada ya wafu kwa ajili ya baba yake (Mzee Moi) aliyeaga dunia Jumanne, Februari 4, 2020.
Wakati akisimulia kuhusu maisha ya marehemu mbele ya mamia ya waombolezaji waliofika Uwanja wa Nyayo, Bw. Gideon alisema, Mzee alitenga muda kukaa na watoto wake na aliwapa maneno ya hekma.
Habari Nyingine: Kalameni amtoroka mke aliyemnyima buyu la asali
Zaidi ya kupenda nyama, Gideon alifichua kuwa, wakati wa kupumzika baba yake alipenda pia kumtizama Muinjilisti Billy Graham kwenye TV, vilevile mieleka huku akimpenda sana mchezaji Shirley Crabtree Junior almaarufu Big Daddy.
Kulingana na seneta, Mzee Moi alimpenda zaidi Big Daddy miongoni mwa wacheza mieleka wa wakati huo.
Habari Nyingine: Biblia na rungu ya Nyayo: Vitu ambavyo viko kando ya mwili wa Moi bungeni
"Wakati anapumzika baada ya kazi kutwa, baba alifurahia kuangalia mieleka kwenye TV na alikuwa shabiki mkubwa wa Big Daddy," Seneta Moi alisema.
Mzee Moi alizikwa nyumbani kwake Kabarnet, Kaunti ya Nakuru kando na kaburi la mke wake Lena.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaX1xgJZmpKihXZa5qrzEp5uaZZuqrq%2BzwKWgmmWdnrKtscqaZKeZXZa5qrfUsJhmq5iWr6q3yGakpK2SrK5uw8BmmaKfXZmupbDYZ5%2BtpZw%3D