EchoVib

Mke wa mfanyabiashara tajiri Simon Kabu alalama kuwa vipusa wanamumezea mate mumewe

Mke wa mfanyabiashara maarufu Simon Kabu amewataka wasichana wenye umri mdogo kuheshimu ndoa za wenyewe

Sarah Kabu alisema anashangazwa na jinsi vipusa wanavyokimbilia kumnyemelea mume wake na wengine bila aibu kutaka kujua siri ya ya kushiriki ngono na mkewe.

Habari Nyingine: Rapa Noti Flow asimulia jinsi alivyomnasa mpenziwe akila uroda na 'Sugar Mummy'

Kulingana na Sarah, kuna wawanawake ambao humtaka Simon awazawadi magari ya kifahari na zawadi zinginezo.

" Wakati wa sherehe za mwaka mpya, nilikuwa napitia akaunti ya Instagram ya mume wangu ambapo nilipata jumbe za baadhi ya wanawake waliomsihi awanunulia magari kama zawadi na wangempatia penzi ambalo hajawahi patiwa, nilishangaa ni vipi wasichana siku hizi hawaheshimu ndoa za wengine," Sarah alisema.

Habari Nyingine: Mshukiwa wa al Shabaab atoroka kwenye kambi Somalia, ajisalimisha kwa polisi Nairobi

Habari Nyingine: Uhuru na Raila wamtoroka DP Ruto, wachagua Tolgos kuongoza BBI Bonde la Ufa

Sarah alisema yeye na mumewe wamekuwa wapenzi wa dhati na huenda hatua ya kuzawadiwa gari peupe ndio iliwafanya baadhi ya wanawake kumtafuta mumewe.

" Mume wangu yuko na password zangu zote za mitandao ya kijamii na pia mimi nina zake, ukimtumia ujumbe lazima nitaupata," Sarah aliongezea.

Sarah na Simon walioana mwaka wa 2009 na kwa pamoja wamejaliwa watoto wawili.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaINzfpJmpKSdXayubrnFmqWymZKerrS0wKuYZqyRn7aztYysoKannmK4oq7UZpilmZyWuqJ5yq6ummWmnr22v8Bmn66lpaKyu7HAZqSarJViura5xLCcZ6Ckork%3D

Jenniffer Sheldon

Update: 2024-09-05