Niko katika hatua za kuacha uraibu wa kunywa pombe kupindukia mpwa wa Uhuru afichua
-Nana Gecaga amedai kuwa anaendelea na hatua za kuacha uraibu wa kunywa pombe kupita kiasi
-Alisema kuwa huo ulikuwa uamuzi wake alioufanya akiwa mchanga kwa msaada na marafiki wachache
-Kulingana na Nana, aliweza kunywa kreti nzima ya bia kwa siku moja
Mpwa wa Rais Uhuru Kenyatta Nana Wanjiru Gecaga alifichua Jumapili, Aprili 8 kuwa alikuwa na mazoea ya kunywa pombe kupita kiasi na kuwa alikuwa katika hatua za kuwacha kunywa pombe kabisa.
Nana ambaye alitimu umri wa miaka 40 Jumapili, Machi 18, 2018 alisema kuwa alifanya uamuzi wa kuacha kunywa pombe pekee yake alipokuwa na miaka 21.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Gavana Mutua amdhihirishia mkewe kuwa ndiye bora kuliko wote, amwonyesha makuu ya dunia
Habari Nyingine: Mama mwenye umri wa miaka 59 ajifungua pacha 4 baada ya kutafuta mtoto kwa miaka nyingi
Mrembo huyo ambaye ni mama wa watoto watatu alidai kuwa angeweza kunywa kreti moja ya bia na chupa moja ya ‘Whiskey’ kila siku.
“Ilikuwa chupa 24 za bia, hiyo ni kreti moja kwa siku na nusu au chupa nzima ya pombe nyingine.” Nana alisema.
Nana ambaye ni mkurugenzi mkuu wa jumba la kimataifa la mikutano ya KICC alikuwa akizungumzia changamoto yake kubwa akisema anaendelea na hatua za kuacha uraibu wa kunywa pombe kupita kiasi.
Habari Nyingine: Picha 16 za kutamanisha zake waziri mchanga wa kike nchini Botswana zinazowazuzua wanaume
Alichukua fursa hiyo kuwapa moyo wale wanaotaabika kuacha kunywa pombe na walio na wakati mgumu katika maisha yao kwa sababu hiyo.
“Ni hatua moja baada ya nyingine, tuna changamoto, tuna mambo tunayokumbana nayo, usichukuwe msimamo wa mawazo ya kitabu kwa kuangalia jalada la kitabu.
“Kitu ninachoweza kuwaambia ni kesho ni siku nyingine ya kuishi, jaribu kutumia siku hiyo vizuri na usiaibike kuomba msaada, Kenya ina misaada mingi, itumie vizuri.” Nana aliongeza.
Habari Nyingine: Uliza mamako! Sabina Chege amkaripia mfuasi wake aliyemuuliza swali tata kumhusu Benson Chacha
Nana aliongeza kuwa furaha yake inatokana na watoto watatu ambao baba yao ni mwanawe askofu Margaret Wanjiru, Peter Kariuki.
Mmoja alizaliwa mwaka wa 2013 muda mfupi baada ya uchaguzi mkuu, wa pili akizaliwa Uingereza mwaka wa 2015 na wa mwisho alizaliwa mwaka wa 2017.
Nana aliwahi kuzua utata aliporipotiwa kumwajiri mfanyikazi wa nyumbani kutoka Uingereza ambaye alikuwa akimlipa KSh 600,000.
Read ENGLISH VERSION
Una taarifa moto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News
Mkenya wa kwanza nchini Marekani aliye na shahada ya uzalifu ya teknolojia ya matibabu ya nyuklia | TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibH13gpNmpaKjn2K4osDIpJhmoJGpwqJ52ZpkpK2RmLWiedSrmKKapWLEonnKrqWyr5FivbC5wZ5kpK2gnrulwcqimGaloKyubsPAZqyhraKqeqKyyJyfrplencGuuA%3D%3D