Mwanamuziki Ljay Maasai aweka mtandaoni picha za kuvutia sana za harusi yake
-Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za injili L Jay Maasai na mpenziwe Ashley hivi majuzi waliibua wivu mitandaoni kwa kuweka picha za harusi yao
-Wawili hao walifanya harusi mwaka jana lakini hawakuweka picha za harusi hiyo mtandaoni
-TUKO.co.ke ilipata picha za harusi hiyo ya kuvutia na ni wazi kwamba harusi hiyo ilikuwa ‘moto’
Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za injili L Jay Maasai na mkewe mrembo Ashley Mutahi hivi majuzi waliibua wivu mitandaoni kwa kuweka picha za harusi yao, mwaka mmoja baada ya kufanya sherehe hiyo kwa siri.
Habari Nyingine: Sosholaiti Risper Faith awatambulisha wazazi wake kwa umma kwa mara ya kwanza( Picha)
TUKO.co.ke inaelewa kuwa wawili hao walioana 2017 baada ya kuwa katika uhusiano kwa miaka miwili.
Mapema, mwanamuziki huyo alikuwa ameweka picha ya mpenziwe mtandaoni na kudokezea harusi.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Katika msururu wa jumbe katika ukarasa wao 'Lekishon .x. Ashley' ulioonekana na TUKO.co.ke, L Jay Maasai alimtaja mpenziwe kama mkakamavu na mwenye upendo mwingi na aliyekaa naye katika hali zote.
L Jay Maasai hatimaye alimwoa Mutahi lakini kwa siri. Hawakuweka picha zozote mitandaoni baada ya harusi hiyo.
Habari Nyingine: Ronaldo awatumia mashabiki wake ujumbe mzito akisherehekea miaka 33
Hata hivyo, waliamua kuweka picha za harusi yao mitandaoni kwa mara ya kwanza.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosSubscribe to Tuko youtube channel to watch more interesting videos
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4J1f5RmpLCZnpa6tsbIpKBmpJqWxm65wJqqmqFdlsSmt8BmpK2ZnpmusLrIZqeim5iWerutjKSsr62knq5uv8CnmGaykWK1or7UrKBmsZGgsm%2B006aj