Mjane wa aliyekuwa naibu wa rais Kijana Wamalwa afariki
-Mjane wa aliyekuwa naibu wa rais marehemu Kijana Wamalwa amefariki
-Kulingana na ripoti kutoka kwa familia ya Wamalwa, Yvonne Wamalwa aliaga dunia akiwa Nanyuki siku ya Alhamisi, Januari 25
-Mumewe marehemu Kijana Wamalwa aliyekuwa naibu wa rais alifariki mwaka wa 2003 na kufanyiwa mazishi ya kitaifa
Yvonne amekuwa akiishi maisha ya utulivu baada ya kifo cha mumewe
Mke wa aliyekuwa naibu wa rais Kijana Wamalwa ameaga dunia.
TUKO.co.ke imepeta habari kuwa Yvonne Wamalwa alifariki Alhamisi, Januari 25 mjini Nanyuki.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Mwanamke aliyedaiwa kwa kulala na Raila Odinga aeleza bayana kilichtokea
Habari Nyingine: Tabia 10 maalum ambazo hutakosa katika familia za Wakenya
Kulingana na kituo cha Radio Jambo, familia ya Wamalwa inaendelea na mipango ya kusafirisha mwili wake hadi jijini Nairobi.
Chanzo cha kifo cha Yvonne Wamalwa hakijabainika.
Habari Nyingine: Msanii Avril Nyambura ni mjamzito, TUKO.co.ke lina ushahidi usiopingika (video)
TUKO.co.ke inaendelea kufuatilia taarifa hii na tunakujuza mengi punde tu tutakapopata habari zaidi.
Habari Nyingine: Kutana na mwanamke mrembo Mkorino anayewakosesha wanaume usingizi
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una taarifa ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Wafuasi wa NASA wahimizwa kususia bidhaa za kampuni ya Haco Higer – Kwenye TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4FyfY9mpKOZnpp6uK2MmqOisZWgwritjKeYopqlYsSiedGaoKxlm563orrAZq6apZGhxKJ5wJ%2BYq6GbnnupwMyl