Polisi watumwa nyumbani kwa wakili kutoka Nyanza aliyetetea ushindi wa Uhuru
- Maafisa wa polisi wametumwa nyumbani kwa PLO Lumumba katika kaunti ya Siaya
- Iliripotiwa kuwa baadhi ya wafuasi wa muungano wa NASA waliudhika kufuatia hatua ya Lumumba kumtetea Uhuru Kenyatta katika Mahakama ya Juu Zaidi
Maafisa wa polisi wamelazimika kuzingira nyumba yake Patrick Loch Otieno Lumumba (PLO Lumumba) baada ya kuzuka kwa vitisho dhidi yake kutokana na hatua yake ya kumtetea Uhuru katika Mahakama ya Juu Zaidi.
Habari Nyingine: Rais ajishaua 'uchi' na kuibua kichaa mitandaoni (picha)
Lumumba ambaye ni mmoja wa mawakili wa IEBC wanaotetea ushindi wa Uhuru Kenyatta anatoka Yimbo, kaunti ya Siaya.
Kwa mujibu wa Standard, hatua yake ya kumtetea Uhuru ilizua tumbo joto miongoni mwa wafuasi wa NASA walioapa kuchoma nyumba yake.
Pakua APP mpya ya TUKO upate habari BURE
Habari Nyingine: Mke wa Ababu Namwamba asutwa vikali mtandaoni kwa kumpongeza wakili wa IEBC
Usiku ule alipokuwa anatoa tetesi zake katika Mahakama ya Juu Zaidi, baadhi ya wafuasi wa NASA walirusha mawe nyumbani kwake.
Pia, wafanya kazi walisema kuwa waliripoti kisa hicho kwa maafisa wa polisi baada ya jirani yake kuwajuza kuwa kulikuwa na njama ya kuiteketeza nyumba yake.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni?Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosSubscribe to Tuko youtube channel to watch more interesting videos
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdian15fJhmp6ikmai2bsPAraymr5Fiu7rBzJuYp6FdoMSiedaaoqKkmWK4tsDOpJhmpqmWu7utjJqjorGVqbK1scBmrKygmaOxqnnWmmSuoKWnwm%2B006aj